Jumamosi 6 Juni 2026 - 23:55
Nafasi na wajibu wa wanawake katika kudhihiri na serikali ya Imam Mahdi (aj) – Sehemu ya kwanza

Hawza/ Wanawake pia, kama ilivyo kwa wanaume katika jamii, wanapaswa kutumia juhudi zao zote katika kutekeleza nafasi zao kwa ajili ya kufanikisha malengo ya Mwenyezi Mungu, bila mchango wao, kutimia ahadi za Mwenyezi Mungu haiwezekani, ndio maana Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaamuru wanaume na wanawake wote wawili kujipamba kwa maadili na thamani za kiroho; kwa sababu ni jamii na watu wema pekee wanaoweza kuwa warithi wa ardhi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, mfululizo wa tafiti za Mahdawiyyah zenye anuani isemayo “Kuielekea Jamii Bora”, zikiwa na lengo la kueneza mafundisho na maarifa yanayohusiana na Imam wa Zama (aj), unawasilishwa kwenu kama ifuatavyo:

Moja ya tafiti zinazohusiana na kudhihiri na serikali ya Imam wa Zama (aj) ni nafasi ya wanawake na namna ya utekelezaji wa jukumu lao katika mchakato wa kudhihiri na serikali ya Mahdawiyyah.

Kwa kuingia katika mjadala huu, tunawasilisha sehemu ya mtazamo wa Qur'ani wa Imam Shahidi, Ayatullah Khamenei, kuhusu nafasi ya kisiasa na kijamii ya wanawake:

"Katika Uislamu, bay'a ya mwanamke, umiliki wa mwanamke, na uwepo wa mwanamke katika nyanja hizi muhimu za kisiasa na kijamii vimethibitishwa:

﴿إِذَا جَائَکَ الْمُؤْمِنَاتُ یُبَایِعْنَکَ عَلَی أَنْ لَا یُشْرِکْنَ بِاللَّهِ﴾


Watakapo kujia wanawake Waumini wanakuahidi ya kwamba hawatamshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote
(Al-Mumtahanah: 12)

Wanawake walikuwa wakija na kumpa Mtume bay'a, Mtume wa Uislamu hakusema kwamba wanaume waje kutoa bay'a, na kwa kufuata wao, chochote watakachokiamua au kukikubali wanaume, wanawake walazimike kukikubali pia; hapana, ilisemwa kwamba; wanawake pia watatoa bay'a, hivyo wao pia wanashiriki katika kuukubali utawala huu na mfumo huu wa kijamii na kisiasa."

(Hotuba katika mkutano na kundi kubwa la wanawake – 30/6/1379 H.Sh.)

"Uislamu unaposema:


﴿وَالْمُؤْمِنُونَ وَالْمُؤْمِنَاتُ بَعْضُهُمْ أَوْلِیَاءُ بَعْضٍ یَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَیَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْکَرِ﴾


"Na Waumini wanaume na Waumini wanawake wao kwa wao ni marafiki walinzi. Huamrisha mema na hukataza maovu"
(At-Tawbah: 71)

Maana yake ni kwamba wanaume Waumini na wanawake Waumini wote wanashiriki katika kulinda mfumo wa kijamii na katika kuamrisha mema na kukataza maovu, hakumtoa mwanamke katika jambo hili, na sisi pia hatuwezi kumtoa, wajibu wa kuiendesha jamii ya Kiislamu na maendeleo yake uko juu ya kila mmoja; juu ya mwanamke na juu ya mwanaume, kila mmoja kwa namna inayolingana na uwezo wake."

(Hotuba katika mkutano na kundi la wanawake wasomi katika mkesha wa kuzaliwa kwa Sayyidah Fatimah (as) – 13/4/1386 H.Sh.)

Pia tunapaswa kukumbusha kwamba: Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Qur'ani Tukufu ametaja majina kumi ya thamani za kiroho ambazo mwanamume na mwanamke ndani yake ni sawa na washirika, hizi ni sifa ambazo bila kujipamba nazo, jamii ile ya Tawhid inayotarajiwa kujengwa chini ya kivuli cha Uislamu haitajengeka kamwe.

﴿إِنَّ الْمُسْلِمِینَ وَالْمُسْلِمَاتِ وَالْمُؤْمِنِینَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَالْقَانِتِینَ وَالْقَانِتَاتِ وَالصَّادِقِینَ وَالصَّادِقَاتِ وَالصَّابِرِینَ وَالصَّابِرَاتِ وَالْخَاشِعِینَ وَالْخَاشِعَاتِ وَالْمُتَصَدِّقِینَ وَالْمُتَصَدِّقَاتِ وَالصَّائِمِینَ وَالصَّائِمَاتِ وَالْحَافِظِینَ فُرُوجَهُمْ وَالْحَافِظَاتِ وَالذَّاکِرِینَ اللَّهَ کَثِیرًا وَالذَّاکِرَاتِ أَعَدَّ اللَّهُ لَهُمْ مَغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِیمًا﴾


"Hakika Waislamu wanaume na Waislamu wanawake, na Waumini wanaume na Waumini wanawake, na wat'iifu wanaume na wat'iifu wanawake, na wasemao kweli wanaume na wanawake, na wanao subiri wanaume na wanawake, na wanyenyekevu wanaume na wanawake, na watoao sadaka wanaume na wanawake, na wanao funga wanaume na wanawake, na wanao jihifadhi tupu zao wanaume na wanawake, na wanao mdhukuru Mwenyezi Mungu kwa wingi wanaume na wanawake, Mwenyezi Mungu amewaandalia msamaha na ujira mkubwa"
(Al-Ahzab: 35)

Wanawake pia, kama wanaume kwenye jamii, wanapaswa kutumia juhudi zao zote katika kutekeleza nafasi yao kwa ajili ya kufanikisha malengo ya Mwenyezi Mungu, Bila mchango wao, kutimia kwa ahadi za Mwenyezi Mungu hakuwezekani, ndiyo maana Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaamuru wote wawili – mwanamume na mwanamke – kujipamba kwa maadili na thamani za kiroho; kwa sababu ni jamii na watu wema pekee wanaoweza kuwa warithi wa ardhi:

﴿وَلَقَدْ کَتَبْنَا فِی الزَّبُورِ مِنْ بَعْدِ الذِّکْرِ أَنَّ الْأَرْضَ یَرِثُهَا عِبَادِیَ الصَّالِحُونَ﴾

“Na hakika tulikwisha andika katika Zaburi baada ya Kumbukumbu, ya kwamba nchi watairithi waja wangu walio wema.’”

(Al-Anbiyaa: 105)

Kwa kuzingatia yaliyotajwa hapo juu, imebainika kwamba wanawake kwenye jamii pia, kama wanaume wana majukumu na wajibu wa jumla katika njia ya kufanikisha malengo ya Mwenyezi Mungu, ambayo wanapaswa kuyazingatia. Ingawa wanawake wanaweza kuwa na nafasi maalumu na za kipekee ambazo tutazizungumzia katika toleo linalofuata.

Utafiti huu unaendelea...

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha